Hamia kwenye habari

Brother Inver Siyukhov

MEI 18, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: MACHI 12, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AMEFUNGWA | Inver Siyukhov Ajazwa Nguvu

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AMEFUNGWA | Inver Siyukhov Ajazwa Nguvu

Machi 7, 2024, Mahakama ya Jiji la Maykop iliyo katika Jamhuri ya Adygeya ilimhukumu Ndugu Inver Siyukhov kifungo cha miaka sita gerezani. Amekuwa mahabusu tangu Aprili 2021 naye ataendelea kubaki kizuizini.

Mfuatano wa Matukio

  1. Aprili 15, 2021

    Alishtakiwa kwamba aliendesha mkutano mtandaoni

  2. Aprili 16, 2021

    Wenye mamlaka walifanya msako kwenye nyumba ya Inver na pia kwenye nyumba za Mashahidi wengine wanne wa Yehova. Alihojiwa na kuwekwa kizuizini

  3. Aprili 17, 2021

    Alipelekwa mahabusu

  4. Agosti 15, 2021

    Alihamishwa na kupelekwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali lililo kilometa 110 kutoka Maykop

  5. Septemba 13, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tuna hakika kwamba ndugu na dada zetu wapendwa walio Urusi wataendelea “kujipatia nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake.”​—Waefeso 6:10.

a Kwa kuwa kwa sasa Ndugu Siyukhov yuko mahabusu, hatukuweza kupata maelezo kutoka kwake.