Hamia kwenye habari

Ndugu Nikolay Saparov akiwa na mke wake, Nataliya (kulia), pamoja na binti yao, Anastasia (kushoto)

NOVEMBA 8, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: JANUARI 22, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AMEFUNGWA | Kusali na Kusoma Biblia Hutokeza Uvumilivu

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AMEFUNGWA | Kusali na Kusoma Biblia Hutokeza Uvumilivu

Januari 17, 2024, Mahakama ya Jiji la Maykop iliyo katika Jamhuri ya Adygeya ilimhukumu Ndugu Nikolay Saparov kifungo cha miaka sita gerezani. Amekuwa mahabusu tangu Machi 2022 naye ataendelea kukaa kizuizini.

Mfuatano wa Matukio

  1. Machi 22, 2022

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa

  2. Machi 23, 2022

    Nikolay alikamatwa kwenye uwanja wa ndege akiwa na mke wake pamoja na binti yao. Baada ya kumhoji, wenye mamlaka walimshtaki kwa madai ya kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali. Kisha wakampeleka kizuizini. Baadaye, nyumba yao ilifanyiwa msako

  3. Machi 24, 2022

    Nikolay alihamishiwa mahabusu

  4. Mei 19, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kumhusu

Mfano mzuri wa familia ya Saparov unatukumbusha kwamba sikuzote Yehova atasikia watumishi wake waaminifu “[wanapolilia] msaada.”​—Zaburi 119:147.

a Makala hii ilipokuwa ikitayarishwa Ndugu Saparov alikuwa mahabusu na hivyo hatukuweza kupata maelezo kutoka kwake.