JULAI 11, 2023 | HABARI ZIMEONGEZWA: NOVEMBA 9, 2023
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU AMEHUKUMIWA | “Yehova Hataniacha Kamwe”
Mahakama ya Wilaya ya Pozharsky iliyo katika Eneo la Primorye ilimhukumu Ndugu Valeriy Vyaznikov kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi sita. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tuna uhakika kwamba ikiwa tutaendelea kutegemea nguvu za Neno la Mungu kama anavyofanya Valeriy, sisi pia tutafaulu kuvumilia majaribu yetu yote.—Waebrania 4:12.
Mfuatano wa Matukio
2018
Wapelelezi walianza kuwachunguza kisiri Mashahidi wa Yehova katika jiji la Luchegorsk. Mtu mmoja alijifanya kwamba anapendezwa na ujumbe wa Biblia lakini kihalisi alikuwa ofisa wa polisi ambaye alikuwa akitafuta ushahidi. Alirekodi kwa siri mazungumzo yake na baadhi ya Mashahidi wa Yehova katika eneo hilo
Julai 16, 2021
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Valeriy. Alishtakiwa kwa madai ya kwamba alikuwa akijaribu kuwahusisha wengine katika utendaji wa shirika lililopigwa marufuku
Desemba 5, 2022
Aliwekewa vizuizi vya kusafiri
Februari 9, 2023
Kesi ya uhalifu ilianza