Hamia kwenye habari

Kutoka kushoto kwenda kulia, safu ya juu: Ndugu Vasiliy Burenesku, Ndugu Viktor Fefilov, Ndugu Igor Kobotov, na Ndugu Igor Petrov. Safu ya chini: Ndugu Leonid Rysikov, Ndugu Igor Trifonov, na Ndugu Pavel Romashov na mke wake, Dada Viola Shepel

JULAI 26, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: DESEMBA 6, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU NA DADA WAHUKUMIWA | Kuvumilia kwa Ujasiri na Shangwe

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU NA DADA WAHUKUMIWA | Kuvumilia kwa Ujasiri na Shangwe

Desemba 5, 2023, Mahakama ya Jiji la Surgut iliyo katika Eneo Lililotengwa la Khanty-Mansi—Yugra iliwahukumu ndugu 17 pamoja na dada mmoja. Miongoni mwao ni Ndugu Vasiliy Burenesku, Ndugu Viktor Fefilov, Ndugu Igor Kobotov, Ndugu Igor Petrov, Ndugu Leonid Rysikov, Ndugu Igor Trifonov, na Ndugu Pavel Romashov na mke wake, Dada Viola Shepel. a Ndugu wote 17 walihukumiwa kifungo cha nje cha kati ya miaka sita na miezi mitatu kufikia kifungo cha miaka saba. Dada Shepel alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitatu na miezi mitatu. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Februari 15, 2019

    Maofisa wa polisi walifanya msako katika nyumba nyingi za Mashahidi wa Yehova jijini Surgut na pia katika majiji yaliyo karibu. Ndugu saba walisema kwamba waliteswa walipokuwa wakihojiwa. Ndugu watatu waliwekwa mahabusu na mwingine aliagizwa kwenda kwenye hospitali ya watu wenye matatizo ya kiakili

  2. Oktoba 3, 2019

    Viktor, Igor Kobotov, Igor Petrov, Leonid, Igor Trifonov, Pavel, pamoja na Viola waliwekwa kwenye orodha ya watu wenye msimamo mkali

  3. Oktoba 10, 2019

    Vasiliy pia aliwekwa kwenye orodha ya watu wenye msimamo mkali

  4. Julai 23, 2020

    Nyumba ya Igor Petrov ilifanyiwa msako kwa mara ya pili, na maofisa wa polisi wakachukua vitu vingine vya kibinafsi

  5. Oktoba 29, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunaamini kwamba hata ndugu na dada zetu wakikabili ‘dhiki, taabu, mateso, au hatari’ Yehova atawaonyesha upendo na atawategemeza ili ‘washinde kabisa.’​—Waroma 8:35, 37.

a b Alidumisha jina lake la awali hata baada ya kufunga ndoa.