Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Ndugu Roman Mareyev; Ndugu Anatoliy Marunov; na Ndugu Sergey Tolokonnikov na mke wake, Mariya

FEBRUARI 10, 2023 | HABARI ZIMEONGEZWA: JULAI 14, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAFUNGWA | Ndugu Watatu Wafikishwa Mahakamani Moscow

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAFUNGWA | Ndugu Watatu Wafikishwa Mahakamani Moscow

Julai 12, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Savelovskiy iliyo Moscow iliwahukumu Ndugu Roman Mareyev kifungo cha miaka minne na miezi sita gerezani, Ndugu Anatoliy Marunov kifungo cha miaka sita na miezi sita gerezani, na Ndugu Sergey Tolokonnikov kifungo cha miaka mitano gerezani. Anatoliy alipelekwa kizuizini mara moja baada ya kutoka mahakamani. Roman na Sergey tayari walikuwa kizuizini.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunashukuru kwa sababu ya mifano mizuri ya imani ambayo Roman, Anatoliy, na Sergey wanatuwekea. Tuna uhakika kwamba hata tukikabili hali ngumu jinsi gani, hatutaogopa “madhara yoyote,” kwa sababu tunajua kwamba Yehova yuko pamoja nasi.​—Zaburi 23:4.

Mfuatano wa Matukio

  1. Oktoba 20, 2021

    Maofisa wa polisi walifanya msako katika nyumba nane za Mashahidi wa Yehova jijini Moscow. Kesi ya uhalifu inaanzishwa dhidi ya Roman, Anatoliy, na Sergey, na wanashtakiwa kwa madai ya kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali na kuwashawishi wengine kushiriki katika utendaji wa shirika hilo. Ndugu wote watatu wawekwa kizuizini.

  2. Oktoba 22, 2021

    Roman na Sergey wapelekwa mahabusu. Anatoliy anawekwa chini ya kifungo cha nyumbani

  3. Juni 17, 2022

    Kesi ya uhalifu yaanza

a Makala hii ilipokuwa ikitayarishwa, Ndugu Tolokonnikov alikuwa mahabusu, hivyo hatukuweza kupata maelezo kutoka kwake. Dada Pankova alidumisha jina lake la awali hata baada ya kufunga ndoa.