Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia, safu ya juu: Ndugu Vyacheslav Boronos, Ndugu Saveliy Gargalyk, Ndugu Yevgeniy Kayryak, na Ndugu Artem Kim. Safu ya chini: Ndugu Sergey Loginov, Ndugu Aleksey Plekhov, na Ndugu Sergey Volosnikov

JULAI 26, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: DESEMBA 6,
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAHUKUMIWA | Sala Inawaimarisha

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAHUKUMIWA | Sala Inawaimarisha

Desemba 5, 2023

Mahakama ya Jiji la Surgut iliyo katika Eneo Lililotengwa la Khanty-Mansi—Yugra iliwahukumu ndugu 17 pamoja na dada mmoja. Miongoni mwao ni Ndugu Vyacheslav Boronos, Ndugu Saveliy Gargalyk, Ndugu Yevgeniy Kayryak, Ndugu Artem Kim, Ndugu Sergey Loginov, Ndugu Aleksey Plekhov, na Ndugu Sergey Volosnikov. Ndugu hao 17 walihukumiwa kifungo cha nyumbani cha kati ya miaka sita na miezi mitatu na miaka saba. Dada alihukumiwa kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu na miezi mitatu. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Februari 15, 2019

    Maofisa wa polisi walifanya msako kwenye nyumba nyingi za Mashahidi wa Yehova jijini Surgut na pia katika majiji yaliyo karibu. Baada ya msako huo, ndugu watatu kutia ndani Sergey Loginov, waliwekwa mahabusu. Baadaye ndugu mwingine aliagizwa kwenda kwenye hospitali ya watu wenye matatizo ya kiakili. Ndugu saba wanaotajwa kwenye ripoti hii waliteswa baada ya kukataa kutoa habari kuwahusu waabudu wenzao

  2. Februari 26, 2019

    Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu iliagiza serikali ya Urusi imwachilie Sergey Loginov ili apate matibabu

  3. Aprili 11, 2019

    Sergey Loginov aliachiliwa kutoka mahabusu

  4. Oktoba 29, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Ndugu zetu wenye ujasiri wanapoendelea kukabiliana na majaribu, tuna uhakika kwamba Yehova anasikiliza sala zao na kuwajibu haraka wanapotaabika.​—Zaburi 69:17.