Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Ndugu Aleksandr Polozov na mke wake, Svetlana; na Ndugu Stepan Shevelev na mke wake, Oksana

JANUARI 24, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: DESEMBA 29, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAMEHUKUMIWA | Ndugu Aleksandr Polozov na Stepan Shevelev Wamepata Baraka Nyingi Licha ya Mateso

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WAMEHUKUMIWA | Ndugu Aleksandr Polozov na Stepan Shevelev Wamepata Baraka Nyingi Licha ya Mateso

Desemba 29, 2023, Mahakama ya Jiji la Norilsk katika Eneo la Krasnoyarsk ilimhukumu Ndugu Aleksandr Polozov na Ndugu Stepan Shevelev. Kila mmoja wao alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka sita. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Oktoba 20, 2019

    Maofisa wa usalama walizunguka kambi katika jiji la Norilsk. Zaidi ya Mashahidi 50 walizuiliwa

  2. Oktoba 26, 2019

    Aleksandr alikamatwa na kuwekwa mahabusu

  3. Januari 21, 2020

    Aleksandr aliachiliwa baada ya kuzuiliwa kwa miezi mitatu hivi

  4. Februari 19, 2020

    Aleksandr aliwekwa kwenye orodha ya watu wenye msimamo mkali na akaunti zake za benki zikazuiliwa

  5. Mei 6, 2021

    Stepan alishtakiwa kwa “kupanga njama ya uhalifu” pamoja na Aleksandr. “Uhalifu” ambao Stepan anadaiwa kuwa alitenda unatia ndani kusali na kuhubiri

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwategemeza ndugu zetu wapendwa ambao kwa uaminifu ‘wanaendelea kufuatia’ uadilifu licha ya mateso.​—Waamuzi 8:4.