Hamia kwenye habari

Ndugu Yevgeniy Bitusov na Ndugu Leonid Druzhinin

NOVEMBA 30, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: DESEMBA 29, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WANAFUNGWA | Sifa Zao za Kiroho Ziliboreshwa

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WANAFUNGWA | Sifa Zao za Kiroho Ziliboreshwa

Mahakama ya Wilaya ya Zeyskiy iliyo katika Eneo la Amur imewahukumu Ndugu Yevgeniy Bitusov na Ndugu Leonid Druzhinin. Ndugu Bitusov alihukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani. Ndugu Druzhinin alihukumiwa kifungo cha miaka sita na nusu gerezani. Walipelekwa kizuizini moja kwa moja kutoka mahakamani.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunajivunia kuwa na ndugu na dada wanaoendelea kujithibitisha kuwa wahudumu wa Mungu kwa uvumilivu na subira yao. —2 Wakorintho 6:3-10.

Mfuatano wa Matukio

  1. Machi 21, 2019

    Maofisa wa polisi walifanya msako katika nyumba kadhaa za Mashahidi wa Yehova zilizo Zeya, kutia ndani nyumba ya Yevgeniy na ya Leonid

  2. Agosti 10, 2020

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa

  3. Oktoba 13, 2020

    Maofisa wa polisi walifanya msako katika nyumba ya Yevgeniy na ya Leonid kwa mara ya pili. Leonid alichukuliwa na kuhojiwa kwa saa mbili

  4. Juni 20, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza