Hamia kwenye habari

Kuanzia kushoto hadi kulia: Ndugu Maksim Amosov, Ndugu Mikhail Gordeev, Ndugu Nikolay Leshchenko, na Ndugu Dmitriy Ravnushkin

FEBRUARI 21, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: JULAI 31, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WATOZWA FAINI | Akina Ndugu Wanaimarishwa Imani Kupitia Msaada wa Waamini Wenzao

HABARI ZA KARIBUNI—NDUGU WATOZWA FAINI | Akina Ndugu Wanaimarishwa Imani Kupitia Msaada wa Waamini Wenzao

Julai 28, 2023, Mahakama ya Jiji la Petrozavodsk katika Jamhuri ya Karelia iliwahukumu Ndugu Maksim Amosov, Ndugu Mikhail Gordeev, Ndugu Nikolay Leshchenko, na Ndugu Dmitriy Ravnushkin. Ndugu hao walitozwa faini ya kati ya rubo 450,000 (dola 4,909 za Marekani) na rubo 500,000 (dola 5,455 za Marekani).

Mfuatano wa Matukio

  1. Julai 31, 2019

    Maofisa wa FSB walifanya msako katika nyumba na maeneo ya kazi ya Mashahidi 16 wa Yehova

  2. Agosti 2, 2019

    Mpelelezi alimwaamuru Maksim asiondoke nchini. Wenye mamlaka walifungua kesi ya uhalifu dhidi ya Nikolay na kumwaamuru asiondoke katika eneo analoishi

  3. Agosti 6, 2019

    Mpelelezi aliwashtaki Maksim na Nikolay kwa “kosa” la kujifunza Biblia

  4. Septemba 5, 2019

    Maofisa wa FSB walimkamata Mikhail akiwa kazini na wakachukua kompyuta yake. Mpelelezi alifungua kesi ya uhalifu dhidi ya Mikhail

  5. Septemba 20, 2019

    Maofisa wa FSB walifanya msako kazini kwa Dmitriy na wakachukua simu yake. Mpelelezi alimhoji Dmitriy kwa saa nne, akafungua kesi ya uhalifu dhidi yake, na akamwaamuru asiondoke katika eneo analoishi

  6. Oktoba 18, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tuna shangwe nyingi kwa sababu ndugu zetu nchini Urusi wanaendelea kutembea katika kweli licha ya mateso.​—3 Yohana 4.

a b Hatukuweza kupata maelezo ya kibinafsi.