Hamia kwenye habari

Ndugu Aleksey Khabarov

SEPTEMBA 1, 2021
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Aleksey Khabarov Anapata Ujasiri Kupitia Sala na Kutegemea Neno la Mungu

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Aleksey Khabarov Anapata Ujasiri Kupitia Sala na Kutegemea Neno la Mungu

Juni 27, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Porkhovskiy ya Eneo la Pskov haikumpata na hatia Ndugu Aleksey Khabarov. Aliondolewa mashtaka yote ya uhalifu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Novemba 26, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Pskov ilichunguza rufaa aliyokata Aleksey. Kesi yake ilirudishwa mahakamani ili kusikilizwa na hakimu mwingine. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu

  2. Septemba 7, 2021

    Mahakama ya Wilaya ya Porkhovskiy iliyo katika Eneo la Pskov ilimhukumu Aleksey kifungo cha nje cha miaka mitatu

  3. Oktoba 29, 2020

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Aleksey ilianza kusikilizwa

  4. Agosti 28, 2020

    Aleksey alishtakiwa rasmi kwamba alishiriki “katika mkutano wa kidini” ambapo waliokuwepo ‘walizungumza kuhusu imani yao, wakasoma Biblia, wakazungumzia mambo kuhusu Maandiko, na kuimba nyimbo za dini’

  5. Februari 7, 2020

    Aleksey alihojiwa mara ya pili. Wakati wa mahojiano hayo, ilifunuliwa kwamba katika mwaka wa 2018 wenye mamlaka walikuwa wakisikiliza na kurekodi mazungumzo yake ya simu

  6. Januari 31, 2020

    Aleksey alishtakiwa kuwa mhalifu

  7. Mei 24, 2019

    Aleksey alimwandikia barua ya kukata rufaa Ofisa Anayeshughulikia Haki za Kibinadamu katika Eneo la Pskov. Aleksey alieleza kwamba yeye si mhalifu, badala yake alikuwa mwamini mnyoofu. Ofisa huyo aliunga mkono kwamba Aleksey alikuwa na haki ya kuwa na imani na kutenda kupatana na imani hiyo

  8. Aprili 3, 2019

    Nyumba ya Aleksey ilifanyiwa upekuzi, baadhi ya vitu vyake vikachukuliwa, naye akahojiwa na maofisa wa usalama

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunakubaliana kabisa na Aleksey kwamba sikuzote Yehova huwasaidia washikamanifu Wake ‘wawe jasiri na wawe na moyo mkuu.’​—Zaburi 27:14.