Hamia kwenye habari

Ndugu Dmitriy Terebilov akiwa na mke wake Irina

AGOSTI 5, 2021
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Dmitriy Terebilov Anakabili Kifungo kwa Mara ya Tano, Lakini Mara ya Kwanza kwa Sababu ya Imani Yake

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Dmitriy Terebilov Anakabili Kifungo kwa Mara ya Tano, Lakini Mara ya Kwanza kwa Sababu ya Imani Yake

Septemba 22, 2022, Mahakama ya Pili ya Kuchunguza Upya Maamuzi ya Mahakama za Chini ya Urusi ilikataa ombi la pili la rufaa la Ndugu Dmitriy Terebilov. Bado yuko gerezani.

Januari 12, 2022, Mahakama ya Eneo la Kostroma ilikataa ombi la rufaa la Dmitriy.

Mfuatano wa Matukio

  1. Septemba 6, 2021

    Mahakama ya Wilaya ya Sverdlovskiy katika jiji la Kostroma ilimhukumu Dmitriy kifungo cha miaka mitatu gerezani. Alipelekwa gerezani moja kwa moja baada ya hukumu kutangazwa

  2. Septemba 8, 2020

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Dmitriy inaanza

  3. Mei 25, 2020

    Dmitriy anashtakiwa rasmi na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Septemba 19, 2019

    Pesa zilizo katika akaunti ya benki ya Dmitriy zinazuiliwa

  5. Juni 13, 2019

    Kesi ya uhalifu inafunguliwa dhidi ya Dmitriy kwa sababu ya kugawa machapisho yaliyopigwa marufuku na kushiriki katika mikutano ya shirika lililopigwa marufuku

  6. Julai 25, 2018

    Nyumba ya Dmitriy inafanyiwa upekuzi yeye na mke wake walipokuwa njiani kutoka kusanyiko la eneo nchini Moldova. Maofisa waliwazuilia na kuwahoji mara tu waliporudi nyumbani

Maelezo Mafupi Kumhusu

Dmitriy anaendelea kuwa na shangwe inayotokana na ‘kushutumiwa kwa ajili ya jina la Kristo,’ nasi tuna uhakika kwamba “roho ya utukufu, yaani roho ya Mungu, inatulia juu” yake.​—1 Petro 4:14.