Hamia kwenye habari

Ndugu Sergey Belousov

APRILI 1, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Sergey Belousov Anatetea Jina la Mungu

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Sergey Belousov Anatetea Jina la Mungu

Aprili 14, 2022, Mahakama ya Jiji la Seversk katika Eneo la Tomsk ilimhukumu Ndugu Sergey Belousov kifungo cha nje cha miaka mitatu. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Julai 14, 2020

    Maofisa wa FSB walivamia nyumba saba, kutia ndani nyumba ya Sergey. Mpelelezi mmoja wa serikali alijifanya anapendezwa na hivyo akarekodi kisiri mkutano wa kutaniko miezi michache kabla ya uvamizi

  2. Machi 25, 2021

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Sergey

  3. Machi 30, 2021

    Sergey alishtakiwa kwa kutegemea taarifa za mpelelezi wa serikali. Sergey alishtakiwa kwa kushiriki utendaji wa kidini kwa njia ya video mtandaoni na pia kwa sababu ya kuimba na kusali kwa Yehova Mungu

Maelezo Mafupi Kumhusu

Kama Sergey, kadiri tunavyolisifu jina la Yehova, tunahakikishiwa kwamba “ataikweza nguvu ya watu wake.”​—Zaburi 148:13, 14.