Hamia kwenye habari

Ndugu Vasiliy Meleshko

AGOSTI 17, 2021
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Vasiliy Meleshko Ndiye Shahidi wa Nne wa Yehova Kushtakiwa na Kuhukumiwa Haraka Katika Eneo la Krasnodar

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Vasiliy Meleshko Ndiye Shahidi wa Nne wa Yehova Kushtakiwa na Kuhukumiwa Haraka Katika Eneo la Krasnodar

Juni 14, 2022, Mahakama ya Nne ya Kuchunguza Upya Maamuzi ya Mahakama za Chini ilikataa rufaa ya pili ya Ndugu Vasiliy Meleshko. Vasiliy bado yupo gerezani kwa sababu ya imani yake.

Mfuatano wa Matukio

  1. Oktoba 7, 2021, Mahakama ya Eneo la Krasnodar ilikataa ombi la rufaa la Ndugu Meleshko. Hukumu yake ya awali itaendelea kutumika

  2. Agosti 11, 2021

    Mahakama ya Wilaya ya Abinskiy katika Eneo la Krasnodar, ilimhukumu Vasiliy kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kesi yake kusikilizwa mahakamani kwa siku mbili. Alipelekwa kizuizini moja kwa moja kutoka mahakamani. Hii ndiyo kesi ya nne ya Shahidi wa Yehova kuharakishwa katika mahakama hiyo a

  3. Agosti 10, 2021

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Vasiliy inaanza. Alipoulizwa na hakimu, kwa ujasiri Vasiliy alijitambulisha kuwa Shahidi anayetenda wa Yehova

  4. Juni 24, 2021

    Mazungumzo kati ya Vasiliy na Ndugu Aleksandr Ivshin yaliongezwa kwenye orodha yake ya matendo ya kihalifu. Mwendesha-mashtaka aliandika kuwa habari iliyohusika katika mazungumzo yao ilikuwa mada za kidini zinazohusiana na “utumishi kwa Yehova Mungu”

  5. Aprili 12, 2021

    Vasiliy alishtakiwa rasmi kwa uhalifu wa “kutoa na kusikiliza hotuba zinazotegemea machapisho ya kidini” na “kushiriki katika mazungumzo ya pamoja ya vitabu vya kidini,” kutia ndani utendaji mwingine

  6. Aprili 7, 2021

    Saa 12:30 asubuhi, maofisa watatu wenye silaha, wapelelezi wanne, na askari wengine wawili waliingia kwa nguvu nyumbani kwa Vasiliy na Zoya Meleshko na kuanza kufanya msako. Baadaye Vasiliy alikamatwa ili akahojiwe. Wapelelezi walimpiga picha akiwa mbele ya nyumba yake na pia mbele ya jengo ambalo hapo awali ndugu zetu walikuwa wakikutania. Wapelelezi walitumia picha hizo kuwa uthibitisho wa kwamba alikuwepo “katika eneo la tukio.” Vasiliy aliamriwa asiondoke eneo hilo

Maelezo Mafupi Kumhusu

Ingawa kesi hiyo iliyoharakishwa na mateso yanayoendelea dhidi ya ndugu na dada zetu nchini Urusi ni “habari mbaya,” tuna uhakika kwamba Vasiliy na familia yake wataendelea kuwa imara na hawatatikiswa, bali ‘watamtumaini Yehova.’​—Zaburi 112:7, 8.

a Machi 30, 2021, Ndugu Oleg Danilov alihukumiwa miaka mitatu gerezani. Februari 10, 2021, Ndugu Aleksandr Ivshin alihukumiwa miaka saba na nusu gerezani. Aprili 6, 2021, Ndugu Aleksandr Shcherbina alihukumiwa miaka mitatu gerezani.