Hamia kwenye habari

Kushoto hadi kulia: Ndugu Vladimir Chesnokov, Vladimir Dutkin, na Valeriy Yakov

JANUARI 7, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Vladimir Chesnokov, Vladimir Dutkin, na Valeriy Yakovlev Wafikishwa Mahakamani kwa Kumwamini Mungu

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Vladimir Chesnokov, Vladimir Dutkin, na Valeriy Yakovlev Wafikishwa Mahakamani kwa Kumwamini Mungu

Aprili 13, 2022, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Chuvash ilikataa rufaa ya Ndugu Vladimir Chesnokov, Ndugu Vladimir Dutkin, na Ndugu Valeriy Yakovlev. Hivyo wanapaswa kulipa faini walizohukumiwa.

Februari 10, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Kalininskiy iliyoko Cheboksary iliwahukumu Ndugu Chesnokov, Ndugu Dutkin, na Ndugu Yakovlev. Ndugu Dutkin alitozwa faini ya rubo 500,000 (dola 6,715 za Marekani), na Ndugu Chesnokov na Ndugu Yakovlev walitozwa faini ya rubo 400,000 (dola 5,372 za Marekani) kila mmoja. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Wakati

  1. Juni 7, 2021

    Vladimir Chesnokov na Valeriy Yakovlev waliongezwa kwenye kesi hiyo ya uhalifu

  2. Desemba 30, 2020

    Vladimir Dutkin alishtakiwa na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  3. Novemba 25, 2020

    Kesi ya uhalifu ilianzishwa dhidi ya Vladimir Dutkin, na baada ya hapo nyumba yake ikafanyiwa upekuzi. Alipelekwa kituoni kuhojiwa

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Kusoma na kutafakari Neno la Mungu lililoongozwa na roho kunasaidia ndugu na dada zetu kukabili changamoto zao za kila siku na kujionea Yehova ‘akiwaficha katika banda lake siku ya msiba.’​—Zaburi 27:5.