Hamia kwenye habari

Safu ya juu (kushoto hadi kulia): Ndugu Vladimir Ermolaev na mke wake, Valeriya; Ndugu Sergey Kirilyuk na mke wake, Olga

Safu ya chini (kushoto hadi kulia): Ndugu Igor Mamalimov na mke wake, Natalya; Ndugu Aleksandr Putintsev na mke wake, Galina

DESEMBA 20, 2021
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Wanne Wanasubiri Matokeo ya Kesi Baada ya Nyumba Zao Kuvamiwa Katika Eneo la Trans-Baikal

HABARI ZA KARIBUNI | Ndugu Wanne Wanasubiri Matokeo ya Kesi Baada ya Nyumba Zao Kuvamiwa Katika Eneo la Trans-Baikal

Septemba 20, 2022, Mahakama ya Eneo la Trans-Baikal ilikataa ombi la rufaa la Ndugu Vladimir Ermolaev, Sergey Kirilyuk, Igor Mamalimov, na Aleksandr Putintsev. Vladimir, Igor, na Aleksandr bado wako gerezani. Sergey hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Juni 6, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Kati ya Chita ilitangaza hukumu ya Vladimir, Sergey, Igor, na Aleksandr. Sergey alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka sita. Vladimir, Igor, na Aleksandr walihukumiwa kifungo cha miaka sita na nusu gerezani. Vifungo vyao vitaanza mara moja.

Mfuatano wa Matukio

  1. Machi 16, 2021

    Kesi inaanza kusikilizwa

  2. Februari 2, 2021

    Vladimir, Sergey, Igor, na Aleksandr walishtakiwa kwamba wanapanga utendaji wa shirika lililopigwa marufuku

  3. Aprili 3, 2020

    Vladimir aondolewa kifungo cha nyumbani

  4. Februari 15, 2020

    Sergey aachiliwa baada ya kuwa mahabusu kwa siku tano

  5. Februari 12, 2020

    Igor na Aleksandr waachiliwa kutoka kizuizini. Sergey alizuiliwa kwa saa 72 zaidi. Vladimir alifungwa kifungo cha nyumbani kwa siku 52

  6. Februari 10, 2020

    Maofisa wa FSB, walifanya msako katika nyumba 50 za Mashahidi wa Yehova, katika Eneo la Trans-Baikal. Msako huu ulitia ndani nyumba za Mashahidi wazee-wazee na walio na ulemavu. Katika familia mmoja, mtoto aliye Shahidi alipigwa mbele ya mama yake na dada yake mdogo. Ndugu mmoja aliteswa. Mwishoni mwa msako huo, maofisa waliwakamata ndugu kumi kutia ndani Igor, Aleksandr, Sergey, na Vladimir

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Na tuwaige ndugu zetu wenye imani yenye nguvu. Kama Danieli na waandamani wake watatu, ndugu hao ‘wameazimia moyoni’ kubaki waaminifu kwa Yehova, licha ya kushinikizwa sana na wenye mamlaka.​—Danieli 1:8.