Hamia kwenye habari

Ndugu Aleksey Smel

FEBRUARI 3, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—OMBI LA RUFAA LAKATALIWA | Ndugu Aleksey Smelov Anapata Msaada Kutoka kwa Yehova Unaomsaidia Kuvumilia

HABARI ZA KARIBUNI—OMBI LA RUFAA LAKATALIWA | Ndugu Aleksey Smelov Anapata Msaada Kutoka kwa Yehova Unaomsaidia Kuvumilia

Septemba 27, 2022, Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Karelia ilikataa ombi la rufaa la Ndugu Aleksey Smelov. Sasa atalazimika kutoa faini.

Aprili 21, 2022, Mahakama ya Jiji la Kondopoga la Jamhuri ya Karelia ilimhukumu Aleksey. Alitozwa faini ya rubo 400,000 (au dola 5,012 za Marekani).

Mfuatano wa Matukio

  1. Julai 23, 2019

    Wenye mamlaka walifungua kesi ya uhalifu dhidi ya Aleksey, wakisema alikuwa mmoja wa viongozi katika shirika la kidini lililopigwa marufuku na kwamba alishiriki kupanga mikutano na “utendaji wa kueneza propaganda”

  2. Julai 31, 2019

    Maofisa wa FSB walivamia nyumba 15 na maeneo ya kazi ya Mashahidi wa Yehova katika majiji ya Kondopoga na Petrozavodsk. Maofisa waliojifanya kuwa mafundi-bomba waliingia kwenye nyumba ya akina Smelov na kufanya upekuzi. Aleksey na mke wake, Irina, walipelekwa kwenye ofisi ya FSB katika eneo hilo na kuhojiwa. Aleksey alipelekwa baadaye kwenye makao makuu ya FSB huko Petrozavodsk. Saa 5:30 usiku aliachiliwa na kuagizwa asiondoke mji wa nyumbani

  3. Agosti 7, 2019

    Wenye mamlaka walimshtaki Aleksey kwa uhalifu chini ya Sehemu ya 1 ya Kifungu Na. 282.2 cha Sheria ya Uhalifu ya Shirikisho la Urusi

  4. Aprili 9, 2020

    Upelelezi ulisitishwa kwa sababu ya janga la COVID-19

  5. Juni 8, 2020

    Upelelezi ulianza tena

Maelezo Mafupi Kumhusu

Kama Aleksey, tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea ‘kudhihirisha nguvu zake kwa niaba’ ya wale wote wanaoteswa.​—2 Mambo ya Nyakati 16:9.