Hamia kwenye habari

Juu kushoto: Ndugu Pyotr Filiznov. Chini kushoto: Ndugu Andrey Vyushin. Kulia: Ndugu Aleksandr Kuznetsov na mke wake, Mariya

FEBRUARI 13, 2023 | HABARI ZIMEONGEZWA: NOVEMBA 6, 2023
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—RUFAA | Familia Tatu Zateswa Jijini Yaroslavl

HABARI ZA KARIBUNI—RUFAA | Familia Tatu Zateswa Jijini Yaroslavl

Oktoba 30, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Dzerzhinsky iliyoko Yaroslavl ilikubali kwa sehemu rufaa ya Ndugu Pyotr Filiznov na Ndugu Andrey Vyushin. Hukumu yao ya kifungo cha nyumbani imepunguzwa kutoka miaka sita na nusu hadi miaka miwili na nusu. Hukumu ya Ndugu Aleksandr Kuznetsov na mke wake, Mariya, haijabadilishwa.

Agosti 3, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Dzerzhinsky iliyoko Yaroslavl imewahukumu Ndugu Pyotr Filiznov; Ndugu Aleksandr Kuznetsov na mke wake, Dada Mariya Kuznetsova; na Ndugu Andrey Vyushin. Kila mmoja wao amehukumiwa kifungo cha nyumbani. Andrey na Pyotr wamehukumiwa miaka sita na nusu. Aleksandr na Mariya wamehukumiwa miaka miwili na nusu. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tuna uhakika kwamba kama tu watumishi hawa wanne wa Yehova ambao ni waaminifu, sisi pia tunaweza kuwa miongoni mwa wale ‘wanaomtumaini Yehova na ambao hawawezi kutikiswa.’​—Zaburi 125:1.

Mfuatano wa Matukio

  1. Aprili 13, 2021

    Wawekwa kizuizini baada ya maofisa wa polisi kufanya msako katika nyumba zao

  2. Aprili 15, 2021

    Wapelekwa mahabusu

  3. Julai 14, 2021

    Waachiliwa kutoka mahabusu na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  4. Septemba 9, 2022

    Kesi ya uhalifu yaanza