Hamia kwenye habari

Kuanzia kushoto hadi kulia: Dada Nadezhda Anoykina, Dada Lyubov Galaktionova, na Dada Nailya Kogay; Ndugu Valentin Osadchuk; na Dada Nina Purge, Dada Raisa Usanova, na Dada Yelena Zayshchuk

SEPTEMBA 23, 2021
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—RUFAA IMEKATALIWA | Dada Sita na Ndugu Mmoja Wanamtegemea Yehova na Waabudu Wenzao Wakati wa Kesi Yao

HABARI ZA KARIBUNI—RUFAA IMEKATALIWA | Dada Sita na Ndugu Mmoja Wanamtegemea Yehova na Waabudu Wenzao Wakati wa Kesi Yao

Septemba 26, 2022, Mahakama ya Eneo la Primorye ilikataa ombi la rufaa ya Dada Nadezhda Anoykina, Lyubov Galaktionova, Nailya Kogay, Nina Purge, Raisa Usanova, na Ndugu Valentin Osadchuk. Wote hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Juni 1, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy iliyoko Vladivostok iliwahukumu Nadezhda, Lyubov, Nailya, Nina, Raisa, Yelena, na Valentin. Akina dada walipewa vifungo vya nje vya miaka miwili. Valentin alipewa kifungo cha nje cha miaka sita. Kwa sasa kesi dhidi ya Dada Yelena Zayshchuk ambaye ana umri wa miaka 87 imeahirishwa kwa sababu yeye ni mgonjwa sana.

Mfuatano wa Matukio

  1. Januari 19, 2021

    Kesi ya uhalifu ilihamishiwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy iliyoko Vladivostok

  2. Novemba 12, 2019

    Kesi ya uhalifu ilirudishwa kwenye ofisi ya mwendesha-mashtaka

  3. Aprili 5, 2019

    Baada ya kuwa mahabusu kwa siku 274, Valentin, ambaye ndiye ndugu pekee aliyehusishwa katika kesi hiyo, aliachiliwa. Aliwekwa chini ya kifungo cha nyumbani

  4. Aprili 19, 2018

    Maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (FSB) walifanya upekuzi katika nyumba saba za Mashahidi

  5. Aprili 9, 2018

    Idara ya Uchunguzi ya FSB katika Eneo la Primorsky ilifungua kesi dhidi ya Valentin na dada hao sita

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunaendelea kutiwa moyo na mifano mizuri ya ndugu na dada zetu wapendwa nchini Urusi. Wanajithibitisha kuwa aina ya watu walio na imani ya kuhifadhi uhai.​—Waebrania 10:39.