MACHI 4, 2022
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—RUFAA YAKATALIWA | Dada Lyudmila Shchekoldina Anaimarishwa na Maneno ya Wengine Yenye Kutia Moyo
Oktoba 6, 2022, Mahakama ya Eneo la Krasnodar ilikataa rufaa ya Dada Lyudmila Shchekoldina. Ataendelea kukaa gerezani.
Mei 23, 2022 Mahakama ya Wilaya ya Pavlovskiy iliyo katika Eneo la Krasnodar ilimhukumu Lyudmila kifungo cha miaka minne na mwezi mmoja gerezani. Hukumu yake ilianza mara moja.
Mfuatano wa Matukio
Aprili 23, 2020
Kesi ya uhalifu ilianzishwa baada ya Lyudmila kuzungumza na mpelelezi kuhusu Biblia bila kujua
Aprili 29, 2020
Wenye mamlaka walifanya msako kwenye nyumba ya Lyudmila kwa saa tisa na kumhoji. Alishtakiwa rasmi kwa kuendeleza utendaji wa shirika lenye msimamo mkali
Juni 21, 2021
Kesi ya uhalifu ilianza
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tuna uhakika kwamba kwa msaada wa Yehova, Lyudmila na ndugu na dada zetu waaminifu wanaokabiliana na majaribu wataendelea kuwa na nguvu.—Zaburi 68:28.