Hamia kwenye habari

Ndugu Aleksandr Nikolayev na mke wake, Yevgeniya

DESEMBA 30, 2021
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—RUFAA YAKATALIWA | Kumtumaini Yehova Kunamsaidia Ndugu Nikolayev Kuwa na Amani

HABARI ZA KARIBUNI—RUFAA YAKATALIWA | Kumtumaini Yehova Kunamsaidia Ndugu Nikolayev Kuwa na Amani

Oktoba 20, 2022, Mahakama ya Eneo la Krasnodar ilikataa ombi la rufaa la Ndugu Aleksandr Nikolayev. Ataendelea kukaa gerezani.

Mfuatano wa Matukio

  1. Desemba 23, 2021

    Mahakama ya Wilaya ya Abinskiy iliyo katika Eneo la Krasnodar ilimhukumu Aleksandr kifungo cha miaka miwili na miezi sita gerezani.

  2. Septemba 30, 2021

    Aliwekwa kizuizini

  3. Agosti 4, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza

  4. Mei 26, 2021

    Anashtakiwa kwa sababu ya kuwa na mazungumzo ya Biblia na familia na marafiki, na wapelelezi wanaona jambo hilo kuwa “kosa la uhalifu dhidi ya misingi ya katiba na usalama wa taifa.”

  5. Aprili 7, 2021

    Saa 12 asubuhi, maofisa wa FSB, wakiandamana na polisi wa kuzuia ghasia, walifanya msako katika nyumba ya familia ya Nikolayev. Walimchukua Aleksandr ili wakamhoji na baadaye wakamwachilia

  6. Machi 31, 2021

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Aleksandr ilianzishwa

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tuna imani kwamba Aleksandr na ndugu na dada zetu wote waaminifu walio Urusi na Crimea, watabarikiwa kwa kuweka tumaini na uhakika wao katika Yehova.​—Yeremia 17:7.