Hamia kwenye habari

JANUARI 27, 2020 | HABARI ZIMEONGEZWA: FEBRUARI 9, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—RUFAA YAKATALIWA | Mahakama ya Urusi Yawahukumu Ndugu Aleksandr Prianikov, Pamoja na Dada Vanera na Darya Dulova

HABARI ZA KARIBUNI—RUFAA YAKATALIWA | Mahakama ya Urusi Yawahukumu Ndugu Aleksandr Prianikov, Pamoja na Dada Vanera na Darya Dulova

Februari 8, 2024, Mahakama ya Eneo la Sverdlovsk ilikataa ombi la rufaa ya Ndugu Aleksandr Prianikov na Dada Venera Dulova. Sasa vifungo vyao vya nje vitaanza kufanya kazi. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu. Kesi dhidi ya Dada Darya Dulova ilifutiliwa mbali kwa sababu alikuwa na umri wa chini ya miaka 18 wakati kosa analoshtakiwa lilipotokea na sheria ya kudhibiti watoto ilikuwa imepitwa na wakati.

Machi 14, 2023, Mahakama Kuu ya Shirikisho la Urusi ilibadili uamuzi wa kufuta hukumu ya kuwaachilia Ndugu Aleksandr Prianikov, Dada Venera na Dada Darya Dulova. Kesi yao sasa itarudishwa kwenye hatua ya kukata rufaa.

Machi 15, 2022, Mahakama ya Eneo la Sverdlovsk ilifuta hukumu dhidi ya Ndugu Aleksandr Prianikov, Dada Venera Dulova, na binti yake Dada Darya Dulova. Hata hivyo, bado wote watatu wanaweza kufungwa kwa sababu ya kesi tofauti.

Januari 27, 2020, Mahakama ya Jiji la Karpinsk iliwahukumu Aleksandr pamoja na Venera na Darya. Wote watatu walihukumiwa kifungo cha nje. Aleksandr alihukumiwa miaka miwili na nusu, Venera miaka miwili, na Darya mwaka mmoja. Ingawa hawatafungwa gerezani, watakuwa chini ya masharti fulani kwa kipindi chote cha hukumu. Watakata rufaa ya uamuzi huo.