OKTOBA 27, 2021
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—RUFAA YAKATALIWA | “Yehova Amekuwa Akinitegemeza”
Novemba 1, 2022, Mahakama iliyo katika Eneo la Primorye ilikataa ombi la rufaa la Dada Liya Maltseva. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.
Septemba 20, 2022, Mahakama ya Jiji la Partizansk iliyo katika Eneo la Primorye ilimhukumu Liya kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi mitatu.
Mfuatano wa Matukio
Juni 22, 2021
Kesi ya uhalifu dhidi ya Liya ilianza
Agosti 18, 2020
Kitengo cha polisi wa siri cha Idara ya Usalama wa Taifa (FSB) kilituma maofisa wake wafanye upekuzi katika nyumba ya Liya. Walichukua Biblia kadhaa, vitabu vya marejeo, na simu yake. Kisha wakampeleka kwenye Idara ya Uchunguzi ili kuhojiwa
Julai 9, 2020
Kitengo cha Huduma za Uchunguzi wa Kifedha cha Kitaifa nchini Urusi kilimweka Liya kwenye orodha ya magaidi na watu wenye msimamo mkali
Juni 1, 2020
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Liya chini ya Sheria ya Uhalifu ya Shirikisho la Urusi. Alishtakiwa kwa kushiriki utendaji wa shirika la kidini lililopigwa marufuku
Maelezo Mafupi Kumhusu
Tunatiwa moyo na mfano mzuri wa Liya katika kuonyesha uvumilivu na tuna uhakika kabisa kwamba Yehova ataendelea kumbariki kwa sababu ya uaminifu wake.—1 Samweli 26:23.