Hamia kwenye habari

Ndugu Aleksandr Kabanov

AGOSTI 8, 2022 | TAREHE YA KARIBUNI: DESEMBA 29, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—UAMUZI WAPINDULIWA | Kujitayarisha Kulimsaidia Aleksandr Kabanov Kubaki Mtulivu

HABARI ZA KARIBUNI—UAMUZI WAPINDULIWA | Kujitayarisha Kulimsaidia Aleksandr Kabanov Kubaki Mtulivu

Desemba 27, 2022, Mahakama ya Eneo la Krasnoyarsk ilipindua kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi sita alichopewa Ndugu Aleksandr Kabanov na ikaomba kesi yake isikilizwe upya. Agosti 5, 2022, Mahakama ya Jiji la Zelenogorsk ilitangaza uamuzi wake katika kesi inayomhusu Ndugu Kabanov lakini alikata rufaa. Amezuiwa kuondoka katika eneo hilo anaposubiri kesi yake isikilizwe upya.

Mahakama ya Jiji la Zelenogorsk iliyo katika Eneo la Krasnoyarsk itatangaza hivi karibuni uamuzi wake katika kesi inayomhusu Ndugu Aleksandr Kabanov. Mwendesha-mashtaka ameomba Aleksandr afungwe kifungo cha miaka miwili na miezi sita gerezani.

Mfuatano wa Matukio

  1. Desemba 26, 2019

    Alikamatwa na akashtakiwa kwa madai ya kushiriki katika utendaji wa shirika lenye msimamo mkali lililopigwa marufuku, kama vile kusoma Biblia na kuzungumza na watu kumhusu Yehova. Aliwekwa mahabusu

  2. Desemba 27, 2019

    Aliachiliwa kutoka mahabusu baada ya hakimu kukataa ombi la mpelelezi kwamba aendelee kukaa mahabusu

  3. Desemba 6, 2021

    Aleksandr alitoa maelezo yake ya mwisho mahakamani. Badala ya kutoa uamuzi, hakimu alirudisha kesi hiyo kwenye hatua ya uchunguzi, na hivyo akarefusha muda ambao kesi hiyo itatumia

  4. Machi 25, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza tena

Maelezo Mafupi Kumhusu

Ndugu na dada zetu nchini Urusi ni mifano mizuri ya imani na wanaishi kupatana na maneno haya ya Isaya 12:2: “Tazama! Mungu ni wokovu wangu. Nitamtumaini nami sitaogopa; Kwa maana Yah Yehova ni nguvu zangu na uwezo wangu.”