Hamia kwenye habari

Ndugu Kirill Yevstigneev

JANUARI 13, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Uhakika Katika Yehova Unamsaidia Ndugu Yevstigneev Kudumisha Uaminifu

HABARI ZA KARIBUNI | Uhakika Katika Yehova Unamsaidia Ndugu Yevstigneev Kudumisha Uaminifu

Agosti 1, 2022, Mahakama ya Eneo la Nizhny Novgorod ilikataa ombi la rufaa la Ndugu Kirill Yevstigneev. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mei 12, 2022, Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy iliyo katika Jiji la Nizhny Novgorod ilimhukumu Kirill kifungo cha nje cha miaka mitatu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Oktoba 8, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza. Katika maelezo yake kwa hakimu, Kirill alieleza kwamba kikusanyiko hicho hakikuwa cha kidini bali kikusanyiko cha kirafiki

  2. Agosti 24, 2021

    Kirill aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  3. Septemba 2, 2020

    Kesi ya uhalifu ilianzishwa dhidi ya Kirill na akashtakiwa “kuunga mkono kifedha utendaji wenye msimamo mkali” kwa sababu alikodisha chumba cha mkutano

  4. Julai 11, 2019

    Wenye mamlaka walimkazia fikira Kirill kwa sababu yeye ndiye aliyetia sahihi mkataba kwa ajili ya chumba cha mkutano; nyumba yake ilifanyiwa upekuzi

  5. Juni 4, 2019

    Uchunguzi ulianzishwa dhidi ya “watu wasiotambulishwa” kwa sababu ya kikusanyiko hicho

  6. Aprili 2019

    Kirill na baadhi ya Mashahidi wa Yehova katika Nizhny Novgorod walikodi chumba cha mkutano kwa ajili ya kikusanyiko cha kirafiki

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tunaendelea kuwa na uhakika tunaposikia kuhusu ujasiri ambao Kirill, mke wake, na ndugu na dada wote waaminifu nchini Urusi na Crimea wanaonyesha licha ya mateso wanayokabili.​—Wafilipi 1:13, 14.