Hamia kwenye habari

Ndugu Vitaliy Omelchenko

OKTOBA 5, 2021
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Ushauri Kutoka kwa Akina Ndugu Unamwimarisha Ndugu Vitaliy Omelchenko Kuvumilia Mateso

HABARI ZA KARIBUNI | Ushauri Kutoka kwa Akina Ndugu Unamwimarisha Ndugu Vitaliy Omelchenko Kuvumilia Mateso

Septemba 22, 2022, Mahakama ya Wilaya katika Eneo la Murmansk ilimhukumu Ndugu Vitaliy Omelchenko. Alitozwa faini ya rubo 500,000 (dola 8,379 za Marekani).

Mfuatano wa Matukio

  1. Januari 29, 2021

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Vitaliy inafikishwa mahakamani

  2. Januari 20, 2020

    Anakamatwa na maofisa wa usalama ili ahojiwe. Alizuiliwa kwa siku mbili kabla ya kuachiliwa. Alizuiwa asiwasiliane na wengine waliohusika katika kesi hiyo na pia asitumie Intaneti

  3. Desemba 23, 2019

    Kamati ya Uchunguzi ya Shirikisho la Urusi katika Eneo la Murmansk ilifungua kesi ya uhalifu dhidi ya Vitaliy. Uhalifu wake ni kushiriki utendaji wa dini yake akiwa Shahidi wa Yehova nyumbani kwake mwenyewe

Maelezo Mafupi Kumhusu

Vitaliy anapoendelea kufaidika kikamili kutokana na mafundisho na faraja kutoka kwa Maandiko, tunatiwa moyo na mfano anaotuwekea.​—Waroma 15:4.