Hamia kwenye habari

Kushoto kwenda kulia: Dada Nadezhda Korobochko, Ndugu Igor Kletkin, na Ndugu Nikolay Kononenko

APRILI 1, 2024 | HABARI ZIMEONGEZWA: JULAI 30, 2024
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—WATATU WAMEHUKUMIWA | “Sitavunja Utimilifu Wangu”

HABARI ZA KARIBUNI—WATATU WAMEHUKUMIWA | “Sitavunja Utimilifu Wangu”

Julai 30, 2024, Mahakama ya Jiji la Nikolaevsk-on-Amur iliyo katika Eneo la Khabarovsk ilimhukumu Ndugu Igor Kletkin na Ndugu Nikolay Kononenko kifungo cha nje cha miaka sita. Dada Nadezhda Korobochko alihukumiwa kifungo cha nje cha miaka mitano. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunamshukuru Yehova kwa kuwatunza kwa upendo na na kuwategemeza wote wanaomtumaini na kutangaza: “Wewe ni Mungu wangu.”​—Zaburi 31:14.

Mfuatano wa Matukio

  1. Oktoba 11, 2021

    Nyumba ya Igor na ya Nadezhda zilifanyiwa msako. Igor aliwekwa kizuizini

  2. Oktoba 12, 2021

    Nadezhda alihojiwa

  3. Oktoba 13, 2021

    Igor aliachiliwa kutoka kizuizini

  4. Oktoba 14, 2021

    Igor na Nadezhda waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  5. Septemba 27, 2022

    Nikolay aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Januari 16, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza