NOVEMBA 28, 2022 | HABARI ZILIONGEZWA: APRILI 27, 2023
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—WATOZWA FAINI | Kumtegemea Yehova Kumeondoa Wasiwasi
Aprili 26, 2023, Mahakama ya Wilaya ya Leninskiy iliyo Nizhny Novgorod iliwahukumu Ndugu Oleg Konshin, Ndugu Sergey Malyanov, Ndugu Roman Zhivolupov a na Dada Svetlana Malyanova, ambaye ni binti ya Sergey. Mahakama iliwatoza faini ya kuanzia rubo 450,000 (dola 5,494 za Marekani) hadi rubo 700,000 (dola 8,546 za Marekani).
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Ndugu na dada zetu wanaoendelea kuwa waaminifu licha ya mateso wanayokabili ni ushahidi hakika wa kwamba wale ‘wanaomtumaini Yehova watakuwa jasiri na wenye moyo mkuu.’—Zaburi 27:14.
Mfuatano wa Matukio
Februari 7, 2019
Hakimu alimruhusu ofisa wa polisi kufuatilia simu ambazo Sergey anapiga na kupokea na hata njia nyingine za mawasiliano ya kielektroni anazotumia
Julai 16-17, 2019
Maofisa wa polisi walifanya msako katika nyumba 31 za Mashahidi wa Yehova wanaoishi katika Eneo la Nizhny Novgorod. Oleg, Sergey, na Svetlana walikamatwa na kupelekwa kizuizini. Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi yao
Julai 18, 2019
Oleg, Sergey, na Svetlana waliruhusiwa kutoka kizuizini. Mahakama iliwazuia ndugu hao wawili kuwasiliana wao kwa wao, kuondoka nyumbani muda fulani, au kutumia Intaneti
Agosti 24, 2021
Roman alishtakiwa rasmi kwa sababu ya kushiriki katika utendaji wa shirika lenye msimamo mkali na akawekewa vizuizi vya kusafiri
Machi 3, 2022
Kesi ya uhalifu ilianza