MEI 3, 2022 | HABARI ZIMEONGEZWA: MACHI 26, 2024
URUSI
HABARI ZA KARIBUNI—WATOZWA FAINI | Sala Iliwaimarisha
Machi 25, 2024, Mahakama ya Wilaya ya Votkinskiy ya Jamhuri ya Udmurtian ilitangaza hukumu ya kumtoza Ndugu Sergey Gobozev faini ya rubo 450,000 (dola 4,855 za Marekani) na kumtoza Ndugu Mikhail Potapov faini ya rubo 400,000 (dola 4,316 za Marekani).
Mfuatano wa Matukio
Januari 20, 2021
Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Sergey na Mikhail, walishtakiwa kwa kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali
Januari 21, 2021
Nyumba ya Sergey ilipekuliwa. Wenye mamlaka walichukua vitu vyake vya kibinafsi, kama vile leseni ya udereva, hati za gari, vifaa vya kielektroni, picha zake, na tafsiri mbalimbali za Biblia. Wenye mamlaka walimkamata Mikhail na kupekua nyumba yake
Januari 22, 2021
Sergey aliwekwa katika kifungo cha nyumbani. Mikhail alipelekwa mahabusu
Mei 18, 2021
Sergey aliondolewa kifungo cha nyumbani lakini akawekewa vizuizi vya kusafiri
Mei 19, 2021
Mikhail aliachiliwa kutoka mahabusu na akawekewa vizuizi vya kusafiri
Oktoba 7, 2021
Kesi ilianza
Maelezo Mafupi Kuwahusu
Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwategemeza Sergey na Mikhail wanapojitahidi kadiri wawezavyo kuimarisha imani yao kupitia funzo la Biblia na sala.—Wakolosai 2:6, 7.