Hamia kwenye habari

Ndugu Dmitriy Semenov na mke wake, Nadezhda

NOVEMBA 4, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI—WENZI WA NDOA WAHUKUMIWA | Waimarishwa na Mifano ya Imani Katika Biblia

HABARI ZA KARIBUNI—WENZI WA NDOA WAHUKUMIWA | Waimarishwa na Mifano ya Imani Katika Biblia

Novemba 8, 2022, Mahakama ya Jiji la Petropavlovsk-Kamchatskiy iliyo katika Eneo la Kamchatka ilimhukumu Ndugu Dmitriy Semenov na mke wake, Nadezhda. Wote wawili walihukumiwa kifungo cha nje cha miaka minne. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Mfuatano wa Matukio

  1. Septemba 3, 2021

    Dmitriy na Nadezhda walizungumza kuhusu Biblia pamoja na mwanamke fulani, lakini mwanamke huyo alianza kutoa habari kwa FSB. Habari hizo zilitumiwa kuanzisha kesi ya uhalifu dhidi yao. Walishtakiwa kwa madai ya kuwashawishi wengine kujiunga na shirika lenye msimamo mkali na kushiriki katika utendaji wake

  2. Septemba 6, 2021

    Msako ulifanywa katika nyumba yao. Walichukuliwa ili wakahojiwe na wakawekewa vizuizi vya kusafiri

  3. Julai 26, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Dmitriy na Nadezhda wanajionea moja kwa moja kwamba Yehova huwasaidia watumishi wake kuwa jasiri na imara wanapokabili mateso. Yeye hawaachi kwamwe.​—Yoshua 1:9.