Hamia kwenye habari

Safu ya juu (kushoto hadi kulia): Ndugu Vyacheslav Ivanov na Ndugu Aleksandr Kozlitin

Safu ya chini (kushoto hadi kulia): Ndugu Sergey Kulakov, Dada Tatyana Kulakova, na Ndugu Yevgeniy Yelin

NOVEMBA 2, 2021
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Waabudu Wenzetu Watano Walioshtakiwa Huko Sakhalin Wanategemezwa na Yehova

HABARI ZA KARIBUNI | Waabudu Wenzetu Watano Walioshtakiwa Huko Sakhalin Wanategemezwa na Yehova

Mei 11, 2022, Mahakama ya Eneo la Sakhalin ilikataa ombi la rufaa ya Ndugu Vyacheslav Ivanov, Ndugu Aleksandr Kozlitin, Ndugu Sergey Kulakov, Dada Tatyana Kulakova, na Ndugu Yevgeniy Yelin. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Januari 31, 2022, Mahakama ya Jiji la Nevelskiy lililo katika Eneo la Sakhalin iliwahukumu Vyacheslav, Aleksandr, Sergey, Tatyana, na Yevgeniy. Sergey na Yevgeniy walipewa vifungo vya nje vya miaka sita na miezi sita. Vyacheslav, Aleksandr, na Tatyana walipewa vifungo vya nje vya miaka miwili.

Mfuatano wa Matukio

  1. Julai 2020

    Vyacheslav, Aleksandr, Sergey, na Tatyana waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  2. Aprili 2020

    Yevgeniy aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  3. Januari 20, 2019

    Maofisa wa kitengo cha polisi wa siri wa Idara ya Usalama wa Taifa (FSB) walivamia nyumba 11 hivi za raia walioshukiwa kuwa Mashahidi wa Yehova. Maofisa hao walitumia nguvu na wakawahoji hata watoto wadogo katika familia hizo. Hilo lilifanyika punde baada ya Rais Vladimir Putin kuahidi kwamba atachunguza kuteswa kwa Mashahidi wa Yehova

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunajua kwamba Yehova ataendelea kuwatunza ndugu na dada zetu wapendwa wanaokubaliana na maneno ya nabii Isaya aliyesema: “Mungu ni wokovu wangu. Nitamtumaini nami sitaogopa.”​—Isaya 12:2.