Hamia kwenye habari

Safu ya juu (kushoto hadi kulia): Ndugu Aleksey Dyadkin, Ndugu Aleksey Goreliy, na Ndugu Nikita Moiseyev

Safu ya chini (kushoto hadi kulia): Ndugu Vladimir Popov, Ndugu Yevgeniy Razumov, na Ndugu Oleg Shidlovskiy

MACHI 24, 2022
URUSI

HABARI ZA KARIBUNI | Yehova Anaendelea Kutegemeza Familia za Ndugu Sita Walio Mahabusu

HABARI ZA KARIBUNI | Yehova Anaendelea Kutegemeza Familia za Ndugu Sita Walio Mahabusu

Septemba 19, 2022, Mahakama ya Jiji la Gukovo iliyo katika Eneo la Rostov iliwahukumu Ndugu Aleksey Dyadkin, Ndugu Aleksey Goreliy, Ndugu Nikita Moiseyev, Ndugu Vladimir Popov, Ndugu Yevgeniy Razumov, na Ndugu Oleg Shidlovskiy. Ndugu Goreliy na Ndugu Shidlovskiy walihukumiwa kifungo cha miaka sita na nusu gerezani. Ndugu Dyadkin, Ndugu Moiseyev, Ndugu Popov, na Ndugu Razumov walihukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani. Hukumu hizo zitatekelezwa mara moja.

Mfuatano wa Matukio

  1. Agosti 8, 2020

    Maofisa wa FSB walifanya msako katika nyumba 17 za Mashahidi wa Yehova katika majiji matatu katika Eneo la Rostov na katika jiji la Kursk. Ndugu Goreliy, Ndugu Moiseyev, Ndugu Razumov, na Ndugu Shidlovskiy walikamatwa na kisha siku iliyofuata walipelekwa mahabusu. Ndugu Popov aliwekwa kwenye orodha ya wahalifu nchini

  2. Agosti 12, 2020

    Maofisa wa FSB walimweka Ndugu Popov kizuizini. Kisha baada ya siku mbili alipelekwa mahabusu

  3. Agosti 21, 2020

    Baada ya Ndugu Dyadkin kuhojiwa na wenye mamlaka alipelekwa mahabusu

  4. Juni 28, 2021

    Wakili aliwatembelea ndugu hao sita wakiwa mahabusu. Walimweleza kuhusu hali ngumu wanazopitia, kama vile joto kali lililozidi nyuzi 40 Selsiasi, kuvu kwenye kuta, na kuwekwa pamoja na wafungwa walio na COVID-19

  5. Julai 21, 2021

    Ndugu Popov alikuwa na matatizo ya kupumua, basi alihamishwa na kupelekwa kwenye mahabusu nyingine yenye kituo cha matibabu. Baada ya muda alipelekwa hospitali

  6. Septemba 30, 2021

    Ndugu Popov alirudishwa mahabusu baada ya kuwa hospitali kwa zaidi ya miezi miwili

  7. Novemba 17, 2021

    Kesi ya uhalifu ilianza, na ndugu hao sita wakaongezewa muda wa kukaa mahabusu

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunaendelea kumwomba Yehova kwa bidii awasaidie ndugu hao na familia zao. Tuna uhakika kwamba Yehova atawapa imani na nguvu wanazohitaji.​—Waroma 15:30.

a b c d e f Kwa sababu ndugu hao sita wako mahabusu kwa sasa, haikuwezekana kuzungumza nao ili kujua maoni yao.