Hamia kwenye habari

Ndugu Aleksey Yershov

NOVEMBA 5, 2021
URUSI

Habari za Karibuni | Ratiba ya Kiroho ya Ndugu Aleksey Yershov Inamsaidia Asivunjike Moyo

Habari za Karibuni | Ratiba ya Kiroho ya Ndugu Aleksey Yershov Inamsaidia Asivunjike Moyo

Aprili 7, 2022, Mahakama ya Eneo la Tomsk ilibadili hukumu iliyokuwa imetolewa dhidi ya Ndugu Aleksey Yershov. Sasa amepewa kifungo cha nje cha miaka mitatu. Aliachiliwa mara moja kutoka gerezani.

Januari 19, 2022, Mahakama ya JIji la Severskiy katika Eneo la Tomsk ilimhukumu Aleksey kifungo cha miaka mitatu gerezani. Hukumu yake ilianza kutekelezwa mara moja.

Mfuatano wa Matukio

Mahakama ya Jiji la Severskiy itatangaza uamuzi wake hivi karibuni katika kesi inayomhusu Ndugu Aleksey Yershov. a Mwendesha-mashtaka aliomba Ndugu Aleksey afungwe kifungo cha miaka mitano.

  1. Juni 22, 2021

    Kesi hiyo ya uhalifu iliwasilishwa kwenye Mahakama ya Jiji la Severskiy iliyo katika Eneo la Tomsk

  2. Machi 30, 2021

    Aleksey alishtakiwa rasmi kwa kosa la uhalifu kwa kutegemea video zilizorekodiwa na mtu ambaye kwa zaidi ya mwaka mmoja alijifanya anapendezwa kujifunza Biblia

  3. Julai 14, 2020

    FSB (polisi wa siri wa Urusi) pamoja na maofisa wa Kamati ya Uchunguzi walivamia na kupekua nyumba ya Aleksey kwa saa saba. Walichukua kadi za benki, vifaa vya kielektroni, Biblia, pasipoti, na vifaa vya kuunganishia Intaneti (Wi-Fi)

Maelezo Mafupi Kumhusu

Kusoma Biblia kila siku pamoja na kusali kutaendelea kuwatia nguvu na kuwafariji ndugu na dada zetu nchini Urusi. Andiko la Zaburi 9:9 linatuthibitishia hivi: “Yehova atakuwa kimbilio salama kwa wanaokandamizwa, kimbilio salama katika nyakati za taabu.”

a Tarehe ya hukumu haitolewi mapema pindi zote.