SEPTEMBA 29, 2020
URUSI
Hakimu Arudisha Mashtaka Dhidi ya Dada Yelena Barmakina kwa Mwendesha-Mashtaka kwa Sababu ya Kukosekana kwa Ushahidi
Septemba 29, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Pervorechenskiy jijini Vladivostok haikutoa hukumu katika kesi dhidi ya Dada Yelena Barmakina. Badala yake, mahakama ilirudisha kesi hiyo katika ofisi ya mwendesha-mashtaka. Hakimu alisema kwamba mwendesha-mashtaka hakuwa na ushahidi wa kutosha wa kuunga mkono madai yake dhidi ya Dada Barmakina ya kuwa na msimamo mkali. Mwendesha-mashtaka anaweza kukata rufaa uamuzi huo. Kwa sasa, kesi hiyo haiendelei mpaka ofisi ya mwendesha-mashtaka itakapotoa ushahidi unaotosha utakaofanya kesi hiyo iendelee kusikilizwa.