Hamia kwenye habari

Watatu kati ya ndugu na dada 80 nchini Urusi ambao wamepewa kifungo cha nje

Oktoba 14, 2021
URUSI

Hali Ikoje kwa Zaidi ya Mashahidi 80 wa Yehova Ambao Wako Katika Kifungo cha Nje?

Hali Ikoje kwa Zaidi ya Mashahidi 80 wa Yehova Ambao Wako Katika Kifungo cha Nje?

Tangu Aprili 2017, Urusi ilipopiga marufuku utendaji wa Mashahidi wa Yehova, zaidi ya ndugu na dada 500 wamekamatwa na kushtakiwa kuwa watu wenye msimamo mkali. Mashahidi 40 hivi wamefungwa gerezani, na wengine 15 wametozwa faini. Zaidi ya Mashahidi 80 wamehukumiwa kuwa wahalifu na kupewa kifungo cha nje. Ingawa kwa sasa hawahitaji kwenda gerezani, hukumu zao si za haki na zina madhara makubwa.

Kulingana na Sheria ya Uhalifu ya Urusi, hakimu ana mamlaka ya kumpa mtu kifungo cha nje badala ya kifungo cha gerezani. Ikiwa hakimu ataamua kufanya hivyo, atamwekea vizuizi mtu aliyeshtakiwa na kumweka chini ya usimamizi wa muda. Ikiwa atakiuka masharti ya usimamizi, mahakama inaweza kumfunga gerezani kwa muda uliotolewa awali wa kifungo cha nje.

Hali ikoje kuishi katika kifungo cha nje? Na Yehova anawasaidiaje ndugu na dada zetu walio chini ya hali hiyo? Tuliwahoji baadhi ya wale ambao wamepewa kifungo cha nje cha miaka miwili hadi sita. Walieleza changamoto wanazokabili na jinsi Yehova amewasaidia kukabiliana nazo.

Nafasi hii ya kuchunguza maisha ya wale ambao wamepewa vifungo vya nje inatuchochea kusali hata zaidi kwa ajili yao na familia zao. Masimulizi yao yanatuthibitishia kwamba Yehova anajibu sala kama hizo na kuwategemeza watumishi wake washikamanifu kupitia majaribu ya namna zote.—2 Wakorintho 1:3, 4.