Hamia kwenye habari

Jopo la majaji watatu katika Mahakama ya Mkoa wa Oryol wakitangaza kuunga mkono hukumu ya Dennis Christensen ya miaka sita

JUNI 11, 2019
URUSI

Hukumu ya Dennis Christensen Kukatiwa Rufaa Kwenye Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu

Hukumu ya Dennis Christensen Kukatiwa Rufaa Kwenye Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu

Kama ilivyoripotiwa, Mei 23, 2019, Mahakama ya Mkoa wa Oryol iliunga mkono uamuzi wa kumfunga Dennis Christensen. Hivyo, Ndugu Christensen bado ana kifungo cha miaka sita. Kwa kuwa amekuwa mahabusu kwa miaka miwili, sheria ya nchi ya Urusi inachukulia muda huo kama miaka mitatu ya kutumikia gerezani, hivyo bado anahitaji kutumikia kifungo cha miaka mitatu. Juni 6, 2019 muda wa jioni, Ndugu Christensen alihamishiwa gerezani ili kuanza kutumikia kifungo chake. Ombi la kupinga kifungo cha uhalifu cha Ndugu Christensen litatumwa kwenye Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR). Ombi la kupinga kuwekwa mahabusu lilishatumwa kwenye ECHR.

Tunavutiwa na jinsi Ndugu Christensen anavyovumilia kwa utulivu ukosefu huu wa haki. Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kumtegemeza yeye pamoja na Mashahidi wa Yehova wengine zaidi ya 200 nchini Urusi waliokabili mashtaka ya uhalifu.—Zaburi 27:1.

Soma alichosema Dennis Christensen mbele ya Mahakama ya Mkoa wa Oryol, Mei 16, 2019.

Soma alichosema Dennis Christensen mbele ya Mahakama ya Mkoa wa Oryol, Mei 16, 2019.