Hamia kwenye habari

Safu ya juu, kuanzia kushoto hadi kulia: Nina Astvatsaturova, Yelena Barmakina, na Ludviga Katanaeva

Safu ya chini, kuanzia kushoto hadi kulia: Igor Lonchakov, Yuriy Redozubov, Yekaterina Treguba, na Yelena Tsorn

JULAI 25, 2023
URUSI

Kusali na Kuwa na Mtazamo Mzuri Kumewasaidia Mashahidi Walio Vladivostok

Kusali na Kuwa na Mtazamo Mzuri Kumewasaidia Mashahidi Walio Vladivostok

Mahakama ya Wilaya ya Pervorechenskiy iliyo Vladivostok itatangaza hivi karibuni hukumu yake katika kesi inayowahusu Dada Nina Astvatsaturova, Dada Yelena Barmakina, Dada Ludviga Katanaeva, Dada Yekaterina Treguba, Dada Yelena Tsorn, Ndugu Igor Lonchakov na Ndugu Yuriy Redozubov. Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunafarijika kujua kwamba Yehova anaendelea kuwabariki na kuwatunza watumishi wake waadilifu na ‘kuwazunguka kwa kibali.’​—Zaburi 5:12.

Mfuatano wa Matukio

  1. Agosti 6, 2019

    Yelena Barmakina ashtakiwa kuwa mhalifu

  2. Juni 8, 2020

    Kesi ya uhalifu yafunguliwa dhidi ya Nina, Ludviga, na Yelena Tsorn

  3. Juni 17, 2020

    Kesi ya uhalifu dhidi ya Yelena Barmakina yaanza

  4. Julai 9, 2020

    Msako wafanywa kwenye nyumba za Nina, Ludviga, Yelena Tsorn, na Yuriy. Yuriy anachukuliwa ili kuhojiwa. Nina, Ludviga, na Yelena Tsorn wanawekewa vizuizi vya kusafiri

  5. Septemba 4, 2020

    Igor ashtakiwa kuwa mhalifu

  6. Septemba 8, 2020

    Yekaterina ashtakiwa kuwa mhalifu

  7. Septemba 29, 2020

    Kesi ya Yelena Barmakina ilirudishwa kwa mwendesha-mashtaka kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kuwa mwenye msimamo mkali

  8. Agosti 11, 2021

    Yuriy ashtakiwa kuwa mhalifu. Kesi ya Yelena Barmakina yafunguliwa upya, kisha kesi zao zinaunganishwa na kusikilizwa kwa pamoja

  9. Septemba 28, 2022

    Kesi ya uhalifu yaanza kusikilizwa

a b Hatukuweza kupata maelezo ya kibinafsi ya Dada Astvatsaturova na Dada Katanaeva.