Hamia kwenye habari

Ndugu Aleksandr Kalistratov

FEBRUARI 20, 2023
URUSI

“Maadamu Yehova Yuko Pamoja Nami, Sikuzote Nitajihisi Nikiwa Nyumbani”

“Maadamu Yehova Yuko Pamoja Nami, Sikuzote Nitajihisi Nikiwa Nyumbani”

Februari 17, 2023, Mahakama ya Jiji la Gorno-Altayskiy iliyo katika Jamhuri ya Altai ilimhukumu Ndugu Aleksandr Kalistratov kifungo cha nje cha miaka sita na nusu. Hahitaji kwenda gerezani wakati huu.

Maelezo Mafupi Kumhusu

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kusikiliza sauti za watumishi wake waaminifu wanapomwita katika nyakati za taabu.​—2 Samweli 22:7.

Mfuatano wa Matukio

  1. 2000

    Alikamatwa kwa sababu ya kukataa kujiunga na utumishi wa kijeshi. Alikaa mahabusu kwa siku 21. Baadaye mahakama iliamua kwamba hana hatia

  2. 2010

    Alishtakiwa kwa madai kwamba alikuwa na msimamo mkali. Kesi yake ilisikilizwa mara mbili kisha ikapelekwa kwenye Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Altai ambayo iliamua kwamba hana hatia

  3. Desemba 16, 2021

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa

  4. Januari 16, 2022

    Maofisa wa FSB walifanya msako katika nyumba tano za Mashahidi wa Yehova katika Jamhuri ya Altai. Maofisa hao walivamia nyumba ya Kalistratov na kumchukua Aleksandr ili kumhoji. Aliachiliwa siku hiyohiyo jioni na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  5. Agosti 25, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianza