Hamia kwenye habari

FEBRUARI 6, 2019
URUSI

Mahakama Nchini Urusi Yamtangaza Dennis Christensen Kuwa na Hatia na Kumhukumu Kifungo cha Miaka Sita

Mahakama Nchini Urusi Yamtangaza Dennis Christensen Kuwa na Hatia na Kumhukumu Kifungo cha Miaka Sita

Februari 6, 2019, mahakama nchini Urusi ilimtangaza Dennis Christensen kuwa na hatia ya “kupanga utendaji wa shirika lenye msimamo mkali.” Amehukumiwa kifungo cha miaka sita gerezani. Atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo isiyo ya haki, ambayo imezungumziwa na vyombo ya habari ulimwenguni pote.

Tutasali kwa ajili ya Dennis Christensen na mke wake, Irina, na ndugu na dada wengi nchini Urusi wanapoendelea “kuwa watulivu na kuwa na tumaini” katika Yehova.—Isaya 30:15.