Hamia kwenye habari

FEBRUARI 14, 2020
URUSI

Mahakama Nchini Urusi Yawatoza Faini Ndugu na Dada Popov

Mahakama Nchini Urusi Yawatoza Faini Ndugu na Dada Popov

Februari 14, 2020, Mahakama ya Jiji la Vilyuchinsk ilimhukumu Ndugu Mikhail Popov na mke wake, Dada Yelena Popova. Mahakama hiyo imemtoza Ndugu Popov rubo 350,000 (dola 5,508 za Marekani) na Dada Popova rubo 300,000. Watakata rufaa ya uamuzi huo.

Mikhail na Yelena walikamatwa Julai 2018. Baada ya muda mfupi waliachiliwa na kusubiri kesi yao ianze.

Tangu 2019, Mahakama nchini Urusi zimewahukumu Mashahidi wa Yehova 28 kwa sababu ya imani yao. Kumi kati yao wamehukumiwa katika kipindi cha miezi miwili tu iliyopita. Hata hivyo, kwa sasa ndugu na dada hao kumi hawajafungwa gerezani.