Hamia kwenye habari

JANUARI 29, 2021
URUSI

Mahakama ya Rufaa Urusi Yaunga Mkono Uamuzi wa Kuwahukumu Mashahidi Sita

Mahakama ya Rufaa Urusi Yaunga Mkono Uamuzi wa Kuwahukumu Mashahidi Sita

Januari 29, 2021, Mahakama katika Eneo la Ulyanovsk imeunga mkono uamuzi uliotolewa Oktoba 2020 uliomhukumu Ndugu Aleksandr Ganin, Khoren Khachikyan, Andrey Tabakov, na Mikhail Zelenskiy, pamoja na Sergey Mysin na mke wake, Nataliya. Urefu wa hukumu za vifungo vya nje walizopewa hautabadilika isipokuwa katika kisa cha Sergey. Mahakama iliongeza urefu wa kifungo chake kutoka miaka minne hadi miaka minne na nusu. Hawatahitaji kwenda gerezani kwa sasa.