Hamia kwenye habari

SEPTEMBA 4, 2020
URUSI

Mahakama ya Rufaa ya Urusi Yakataa Kumwachilia Mapema Ndugu Christensen, Yaagiza Mahakama ya Awali Imhukumu Upya

Mahakama ya Rufaa ya Urusi Yakataa Kumwachilia Mapema Ndugu Christensen, Yaagiza Mahakama ya Awali Imhukumu Upya

Septemba 4, 2020, Mahakama ya Eneo la Kursk ilifutilia mbali uamuzi wa Juni 23 wa Mahakama ya Wilaya ya Lgov wa kumwachilia mapema Ndugu Dennis Christensen. Mahakama ya Eneo la Kursk iliagiza Mahakama ya Wilaya ya Lgov itumie hakimu mwingine kusikiliza upya kesi hiyo. Tarehe haijawekwa ya kusikiliza upya kesi hiyo.