Hamia kwenye habari

FEBRUARI 26, 2021
URUSI

Mahakama ya Rufaa ya Urusi Yapunguza Kifungo cha Ndugu na Dada Rayman

Mahakama ya Rufaa ya Urusi Yapunguza Kifungo cha Ndugu na Dada Rayman

Februari 26, 2021, Mahakama ya Eneo la Kostroma iliunga mkono uamuzi uliotolewa Oktoba 2020 wa kumfunga Ndugu Sergey Rayman na mke wake, Valeriya. Lakini mahakama ilipunguza muda wa vifungo vyao. Kifungo cha nje cha Sergey kilipunguzwa kutoka miaka minane na kuwa miaka mitatu, na kifungo cha Valeriya kilipunguzwa kutoka miaka saba na kuwa miaka miwili. Hawahitaji kwenda gerezani wakati huu.