Hamia kwenye habari

APRILI 1, 2020
URUSI

Mahakama ya Urusi Imeamua Kumfunga Ndugu Igor Ivashin, Kifungo cha Nje cha Miaka Sita

Mahakama ya Urusi Imeamua Kumfunga Ndugu Igor Ivashin, Kifungo cha Nje cha Miaka Sita

Aprili 1, 2020, Mahakama ya Wilaya ya Lensky iliyo katika Jamhuri ya Sakha imeamua kwamba Ndugu Igor Ivashin atafungwa kifungo cha nje kwa miaka sita kwa sababu ya imani yake. Ingawa alirudi nyumbani baada ya hukumu yake kutolewa, wakati wowote ule atakapoenda kinyume na sheria inayokataza kushiriki mambo ya kidini na inayokataza kufanya ibada, atapelekwa gerezani moja kwa moja. Ndugu Ivashin atakata rufaa.