SEPTEMBA 28, 2021
URUSI
Mahakama ya Urusi Imetupilia Mbali Rufaa Dhidi ya Uamuzi wa Kupiga Marufuku Programu ya JW Library
Septemba 27, 2021, Mahakama ya Jiji la Saint Petersburg ilikataa ombi la rufaa dhidi ya uamuzi wa Machi 31, 2021, uliotangaza kwamba programu ya JW Library ni yenye msimamo mkali na kupiga marufuku isitumiwe kotekote katika Shirikisho la Urusi na Crimea. Uamuzi wa awali wa Mahakama utaanza kutumika mara moja.