Hamia kwenye habari

Ndugu Valeriy Moskalenko akiwa kwenye chumba cha mahabusu katika mahakama wakati wa mojawapo ya vikao vya mwisho vya kesi yake

AGOSTI 30, 2019
URUSI

Mahakama ya Urusi Itatoa Uamuzi Dhidi ya Ndugu Moskalenko Juma Lijalo

Mahakama ya Urusi Itatoa Uamuzi Dhidi ya Ndugu Moskalenko Juma Lijalo

Hakimu Ivan Belykh wa Mahakama ya Wilaya ya Zheleznodorozhniy huko Khabarovsk amepanga kutoa uamuzi mnamo Septemba 2, 2019 katika kesi ya uhalifu dhidi ya Ndugu Valeriy Moskalenko mwenye umri wa miaka 52.

Ndugu Moskalenko amekuwa kizuizini tangu alipokamatwa asubuhi ya Agosti 2, 2018, askari wa Federal Security Service (FSB) na polisi wa kupambana na ghasia walipovamia nyumba yake. Maofisa hao walifanya msako katika nyumba ya Ndugu Moskalenko kwa muda wa saa tano kabla ya kumkamata. Kwa vile amekuwa kizuizini kwa zaidi ya mwaka mmoja, inaelekea kwamba atapatikana na hatia na kuhukumiwa kufungwa gerezani kama ilivyokuwa katika kesi ya Dennis Christensen.

Mnamo Desemba 18, 2018, kesi ya malalamiko ya Moskalenko dhidi ya Urusi, iliwasilishwa katika Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR). Zaidi ya kesi 50 dhidi ya Urusi zimewasilishwa, na tayari serikali ya Urusi imefahamishwa kuhusu kesi 34 kati ya hizo.

Tunajivunia ndugu na dada zetu wapendwa nchini Urusi ‘kwa sababu ya uvumilivu na imani yao katika mateso yao yote na taabu wanayopata.’ Ni wazi kwamba Yehova anawaunga mkono na kuwabariki. Tunasali kwamba aendelee kumpa Ndugu Moskalenko nguvu anazohitaji ili kuvumilia kwa shangwe, bila kujali uamuzi utakaotolewa juma lijalo.—2 Wathesalonike 1:4.