Hamia kwenye habari

FEBRUARI 24, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yahukumu Ndugu Roman Baranovskiy na Mama Yake Mwenye Umri Mkubwa, Dada Valentina Baranovskaya, Wafungwe Gerezani

Mahakama ya Urusi Yahukumu Ndugu Roman Baranovskiy na Mama Yake Mwenye Umri Mkubwa, Dada Valentina Baranovskaya, Wafungwe Gerezani

Februari 24, 2021, Mahakama ya Jiji la Abakan ya Jamhuri ya Khakassia ilimhukumu Ndugu Roman Baranovskiy kifungo cha miaka sita gerezani. Pia, mahakama ilimhukumu mama ya Roman, Dada Valentina Baranovskaya, kifungo cha miaka miwili gerezani. Hii ndiyo mara ya kwanza ambayo mmoja wa dada zetu nchini Urusi amehukumiwa kifungo gerezani kwa sababu ya imani yake. Aprili 2021, Valentina atafikisha umri wa miaka 70 na alipatwa na kiharusi mnamo Julai 2020.

Baada ya uamuzi kutangazwa, wote wawili walipelekwa kizuizini. Rufaa itakatwa ya uamuzi huo.