Hamia kwenye habari

FEBRUARI 26, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yakataa Kumwachilia Mapema Ndugu Aleksey Miretskiy

Mahakama ya Urusi Yakataa Kumwachilia Mapema Ndugu Aleksey Miretskiy

Februari 26, 2021, Mahakama ya Wilaya ya Kati Huko Orenburg ilikataa ombi la kumwachilia mapema Ndugu Aleksey Miretskiy. Alikuwa mmoja kati ya ndugu watano waliopigwa wakiwa gerezani mnamo Februari 2020. Aleksey ametumikia zaidi ya nusu ya kifungo chake.