Hamia kwenye habari

FEBRUARI 25, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yakataa Kumwachilia Mapema Ndugu Roman Gridasov

Mahakama ya Urusi Yakataa Kumwachilia Mapema Ndugu Roman Gridasov

Februari 25, 2021, Mahakama ya Eneo la Orenburg ilikataa ombi la kumwachilia mapema Ndugu Roman Gridasov. Ataendelea kuwa gerezani hadi Agosti 2021 kifungo chake kitakapokwisha. Amekuwa gerezani tangu Septemba 2019. Roman alikuwa kati ya ndugu watano waliopigwa na walinzi wa gereza mnamo Februari 2020.