Hamia kwenye habari

APRILI 22, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yakataa Ombi la Rufaa la Dada Reyno-Chernyshova

Mahakama ya Urusi Yakataa Ombi la Rufaa la Dada Reyno-Chernyshova

Aprili 22, 2021, mahakama ya Eneo Lililotengewa Wayahudi ilikataa ombi la rufaa la Dada Yelena Reyno-Chernyshova. Badala yake, mahakama ilikubali ombi la mwendesha-mashtaka la kuongeza hukumu aliyopewa awali ya faini ya rubo 10,000 (dola 135 za Marekani), na kumpa kifungo cha nje cha miaka miwili na miezi sita. Hatahitaji kwenda gerezani wakati huu.