Hamia kwenye habari

APRILI 15, 2021
URUSI

Mahakama ya Urusi Yakataa Ombi la Rufaa la Ndugu Aleksandr Ivshin

Mahakama ya Urusi Yakataa Ombi la Rufaa la Ndugu Aleksandr Ivshin

Aprili 15, 2021, Mahakama ya Eneo la Krasnodar iliunga mkono uamuzi wa kwamba Ndugu Aleksandr Ivshin afungwe gerezani kwa miaka saba na nusu. Anapaswa kukaa gerezani. Hiyo ndiyo hukumu kali zaidi ambayo yeyote kati ya Mashahidi wa Yehova amewahi kupewa tangu tengenezo letu lilipopigwa marufuku mnamo 2017.